HAKIKA HII TABIA ILIYOFANYWA NA ALIYEKUWA MUME WA JESSICA INAPASWA KUKOMESHWA MALA MOJA`

Jessica Kikumbi
JESSICA AKIWA NA MUMEWE ENZI NA KABLA YA KUTENGANA
Jessica Kikumbi
JESSICA KIKUMBI

Kutokana na Kuenea kwa kasi kwa matumizi ya Mtandao hapa nchini. Tanzania kumefanya watu wengi wajikite katika kutumia Mitandao. Japo kuwa kuna aina mbalimbali za Matumizi kuna wanao tumia kwa faida na wanaotumia kwa matumizi mabaya.

Kutokana na Mwanadada Jessica Kikumbi akimshutumu mumewe Kusambaza Picha zake katika mitandao mbalimbali hapa nchini kwa Lengo la Kumchafua. 

Mtandao Huu una laani Vikali Tabia hii ya kusambaza Picha Kwa lengo la kumchafua mtu.

Tabia hii Hujitokeza pindi tu wapenzi wanapohitalifiana na kuamua kuchukua hatua ya kuachana, Haakika kwa mtu anayefanya vitendo vya namna hii lazima atakuwa ni LIMBUKENI na lazima atakuwa na matatizo kichwani kwani Mtu mwenye akili Timamu Hawezi weka Picha za Mtu yeyote mtandaoni kwa nia ya Kumchafua.

Maswali tunayojiuliza kutokana na watu wa namna hii ni ::
  1. DHUMUNI LAO HASA NI LIPI?
  2. WANAFAIDIKA NA KITU GANI ?
  3. WAKIMCHAFUA MWENZAO WANAFAIDIKA NA NINI 
Nanyie akina Dada pia Acheni kuhadaika kwa Kukubali kupiga Picha chafu za namna hizo kwani Utaepukana na watu wanamna hii pindi utakapo vunja mahusiano.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post