VIDEO: NUH MZIWANDA ATUPA KIJEMBE KINGINE KWA SHILOLE

Wahenga wanasema “kila mwamba ngoma huvutia upande wake” msemo huo hauna utofauti mkubwa sana na msimamo wa msanii wa Bongo FLeva hitmaker wa ngoma ya Jike Shupa Nuh Mziwanda.
Nuh Mziwanda na Nawal
Ni baada ya kufunguka kwenye kipaza cha Lindiyetu.com kuwa anamuona mke wake bibie Nawal kuwa ndiye mwanamke wake bora kabisa kati ya wote ambao amewahi kuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi.

Mziwanda ametolea ufafanuzi kauli yake hiyo na kudai kuwa ubora wa mwanamke huyo unakuja pale anapokuwa anajali kazi yake bila kuweka wivu mbele.
“Mwanamke wangu anajua kunitreat vizuri, mpole, mstaarabu, ananisikiliza, ananiachia nifanye kazi tofauti na zamani ambapo nilikuwa nikienda kwenye show lazima unikute na bodyguard pembeni.”

Hayo ni baadhi tu ya maneno na sifa ambazo Nuh Mziwanda amemmwagia baby mama wake Nawal. Kusikiliza full interview bonyeza play kwenye hii video hapa chini.

Unaweza Ku-SUBSCRIBE kwenye Youtube Chanel yetu ili usipitwe na chochote, BOFYA HAPA

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post