MKUU WA MKOA wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ametoa wiki mbili kwa wakazi wa jimbo la Ruangwa kuhakikisha kuwa wanajenga vyoo ili kujiepusha na ugonjwa wa kipindupindu.
Mkuu wa Mkuo wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi
Amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Joseph Mkirikiti afanye msako wa nyumba kwa nyumba ifikapo Januari 15, 2017 na endapo atakuta kuna mkazi wa kijiji chochote hajajenga choo, basi atozwe faisi ya sh. 50,000 mara moja.
Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Desemba 28, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi na Chibula wilayani humo ambako alikuwa akiwasalimia wananchi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu azungumze na wakazi wa vijiji hivyo.
Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na ameamua kutumia muda huo kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema wakulima wengi wamevuna korosho msimu na baadhi yao wamelipwa vizuri, hivyo hawana budi kutumia sehemu ya fedha hizo kujenga vyoo ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na hasa kipindupindu.
“Hili ni agizo la Serikali siyo langu binafsi kwa hiyo ni amri halali. Kikilipuka kipindupindu, naanza na Mkuu wa Wilaya kabla na mimi sijaulizwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu au Mheshimiwa Rais,” amesema.
Katika hatua nyingine, Bw. Zambi amewahimiza wakazi wa vijiji hivyo wapande miche ya mikorosho katika msimu huu wa kilimo pindi mvua zitakapoanza kwani iliyopo imekaa kwa zaidi ya miaka 50 na sasa haizai matunda ya kutosha.
“Mkoa wetu una mpango wa kubadilisha miti ya mikorosho kwani mingi ni ya zamani na imekaa kwa zaidi ya miaka 40 hadi 50 na hivi sasa haina tija kwenye mazao yake. Mti mzuri wa korosho unazaa hadi kilo 40 lakini hii iliyopo sasa hivi inatoa kilo 10 tu,” amesema.
Amesema Serikali imeagiza kila kijiji kiandae miche 5,000 kwa mwaka na kuwapa wananchi kwa bei nafuu na mpango huo tumeshaanza kuutekeleza.

Wananchi wa Ruangwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Lindi akitoa agizo hilo.

BOFYA PLAY HAPA CHINI KUANGALIA MKUTANO HUO.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.