JE SKENDO NDIZO ZIMEMFANYA WEMA SEPETU AFIKIRIE KUKIMBILIA KENYA? JIBU LIKO HAPA

Pengine Wema Sepetu amechoshwa na maisha ya skendo akiwa Bongo na sasa ameanza kufikiria kuanzisha maisha katika nchi nyingine, mbali kidogo na nyumbani.
Wema Sepetu
Walau kwa alichosema kupitia post yake ya Instagram, Miss Tanzania huyo wa zamani na muigizaji wa filamu, inaonekana kuwa Kenya inaweza kuwa ‘destination’ iliyopata kura nyingi.

Mrembo huyo yupo jijini Nairobi, Kenya alikoalikwa kwenye kiota cha Xsmillionaires kuhost shughuli ya ulaji bata ya Powerball Thursdays.
Wema Sepetu
“Wow….!!! I cant start to tell you How excited I am for Tomorrow. Finally I get to Chill, Dance & Mingle with my Kenyan darlings. The Only Place to start Our Weekend is at @xsmillionaires @xsmillionaires,” aliandika.

“Oh nd Did I mention I’m thinking of Moving To Nai……. Well Let me Nat say Much… Cant wait to See you Guys,” ameongeza.

Anaweza akawa ameongea kwa kuchombeza tu lakini ukweli ni kwamba Wema ni maarufu sana nchini Kenya, asante kwa uhusiano wake na Diamond na Idris Sultan. By the way wakati Wema akitarajiwa kuhost shughuli hiyo huko Nairobi, ex wake Idris yupo jijini Kampala ambako naye atakuwa host kwenye tuzo za ASFAS.
******

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post