
Siku chache baada ya Super Star Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari the Bosslady kupata mtoto wa pili ambaye alizaliwa December 6, 2016 tayari mtoto huyo ameanza kuzichukua headlines baada tu yakupewa jina na kufunguliwa akaunti ya Instagram ambayo mpaka kufikia muda inaandikwa taarifa hii imefikisha followers zaidi ya 27.7 elfu.
Zari alijifungua saa 10:35 alfajiri katika Hospitali ya Netcare Pretoria South Africa, Pamoja na kuwaomba mashabiki wake kumsaidia kupata jina la mtoto wake ambaye ni wa wakiume, Diamond na Zari wameamua kumuita mtoto huyo jina la Riaz Nasib Abdul huku ikisemekana kuwa ni kinyume cha jina la Zari “Riaz”.

Ikumbukwe kuwa mtoto wa kwanza Diamond na Zari, Princes Tiffah amefikisha followers zaidi ya milioni 1 na kuwa mtoto wa kwanza barani Afrika kuweka rekodi hiyo.

*********
Tags
WATU MAARUFU