TALAKA YA KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST INANUKIA BAADA YA TUKIO HILI

Kim Kardashian na Kanye West
Kim Kardashian na mume wake Kanye West wameripotiwa kuelekea kutengana na hata Kim K kudai talaka yake baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka miwili na nusu.

Kwa mujibu wa Us Weekly Kim K ametajwa kuwa yeye ndio anataka talaka hii na itakuwa talaka yake ya tatu baada ya kuachana na Damon Thomas na mcheza kikapu Kris Humphries.

Kim Kardashian na Kanye West
Watu wa karibu na Kim K wanasema ni kweli ana taka talaka na haki zote za malezi ya watoto wao wawili ambao ni North ‘3’ na Saint mwenye mwaka mmoja.

Kim K amekaa mbali na Kanye West kwa muda sasa toka aruhusiwe kutoka hospitalini baada ya kupata matatizo ya akili na msongo wa mawazo.

********

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post