HABARI ZA HIVI PUNDE: MBUNGE WA MBEYA "SUGU" ANUSURIKA KIFO

Joseph Mbilinyi "sugu"Taarifa zilizoripotiwa na kituo cha runinga cha ITV leo December 17 2016 zinasema kuwa mbunge wa Mbeya mjini "CHADEMA", Joseph Mbilinyi amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Iyunga jijini Mbeya baada ya gari lake kufeli break na kumgonga mtoto mwenye umri wa miaka 15 ambaye amefariki wakati akipelekwa hospitali.

Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa askari polisi wanne wamejeruhiwa baada ya kupata ajali wakati wakielekea kwenye ajali hiyo aliyopata mbunge Joseph Mbilinyi "sugu"

Gari hilo lilikuwa linaendeshwa na dereva wake, Gabriel Andrew (43) ambaye anashikiliwa na polisi.


******************

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post