Mkongwe kwenye tasnia ya muziki nchini na aliyekua mgombea wa ubunge kupitia chama cha ACT wazalendo, Suleiman msindi maarufu kama Afande Sele mapema hii leo ametangaza kujivua uanachama wa chama cha ACT wazalendo, kupitia ukurasa wake wa Facebook Afande sela kaandika hivi:
"Habari za wkt huu akina ndugu nyote,naamini tupo pamoja ktk kujitafutia maisha na kulijenga taifa letu pendwa Tz ambalo ndani ya katiba yake kuna kipengele muhimu kinachotupa UHURU kwa kila mtu kufanya mambo yake apendavyo ilimradi tu havunji sheria za nchi….sasa kwa kuzingatia UHURU huo tuliopewa na KATIBA yetu mimi Leo natangaza rasmi kujivua uanachama wa chama cha ACT-Wazalendo na kutokua mfuwasi wa chama chochote cha Siasa bali nitabaki kuwa raia wa kawaida ndani ya nchi yetu huku nikiendelea na majukumu yangu mengine ya kimaisha mpaka hapo nitakavyoamua vingine kama nitakua na sababu ya kufanya hivyo…Nawatakia kila la kheri wote waliobaki ndani ya chama pia nawatia moyo mkuu wa kuendeleza harakati za ujenzi wa chama ili kuleta upinzani sahihi na imara utakaosaidia kujenga taifa kwa faida yetu na vizazi vijavyo…naomba ieleweke kuwa uamuzi huu’tarajiwa’sijauchukua kwa bahati mbaya hivyo naomba kila mmoja awe wa ndani au wa nje ya chama chetu aheshimu uamuzi wangu kama mimi ninavyoheshimu maamuzi ya watu wengine kwa mujibu wa KATIBA ya nchi inavyosema…Ahsanteni sana wadau tukutane MAISHANI..."
**************
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.