Unknown Unknown Author
Title: DIAMOND PLATNUMZ HATIMAE AMETOA YA MOYONI KUHUSU BOB JUNIOR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hivi uliwahi kufikiria kuwa licha ya kutemana katika kazi lakini Diamond Platnumz bado anathamini mchango na uwezo mkubwa wa Bob Junior ....
Hivi uliwahi kufikiria kuwa licha ya kutemana katika kazi lakini Diamond Platnumz bado anathamini mchango na uwezo mkubwa wa Bob Junior.
Diamond Platnumz and Bob Junior


Akiongea kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz kinacho hostiwa na Salama Jabri, Diamond alieleza mambo muhimu aliyofanyiwa na Bob Junior katika harakati zake za Muziki.

Lindiyetu.com inakusogeza karibu na Interview hiyo kama uliikosa kuitazama na haya ndio maneno ya moyoni jinsi Diamond Platnumz anavyojivunia kwa kuanza kufanya kazi na Bob junior

“Kiukweli Bob Junior ana mchango mkubwa sana katika katika maisha yangu kwa sababu ukiangalia nyimbo zangu zote zilizonitoa ni yeye ndiye alikuwa ametengeza. Japokuwa hata kipindi ambacho nilikuwa nazitengeneza inawezekana watu walikuwa hawajamuona kama anaweza kuwa producer mzuri sana. Lakini mimi nilikuwa naona mbona huyu natoka naye, nakufa naye mimi yaani huyu natoa nyimbo na inahit,” aliongeza.
Kuna mengi yamemkuta pia Chibu lakini hakusita kusema pia harakati alizopitia kwenye maisha yake ya mziki.
“Nakumbuka tulifanya nyimbo kama sita, Nenda Kamwambie, Mbagala, Nitarejea, Binadamu, nyimbo tofauti tofauti. Kila nyimbo alikuwa akinitengenezea akinipa beat nikifika nyumbani naandika vibaya sana. Na mpaka nakumbuka ilifika time niliweka kama chuki fulani kwa wasanii waliopo pale wakaona mbona unampendelea mtu fulani, yeye akasema mimi ni producer, natengeneza beat nikimpa msanii kaandikie kitu kikali, akasema huyu nikimpa analeta beat kali.” Alisema Diamond.
*********** 

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top