Unknown Unknown Author
Title: CHODAWU: SERIKALI RIDHIENI MKATABA WA WAFANYAKAZI WA NDANI ILI KURUDISHA HESHIMA NA HAKI ZA MSINGI KWA JAMII
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
NA Elizabeth Vicent, Dar es Salaam SERIKALI imeombwa kuridhia mkataba wa Shirika la Kazi duniani (ILO) namba 189 unaohusu kundi la wafanyak...
NA Elizabeth Vicent, Dar es Salaam
SERIKALI imeombwa kuridhia mkataba wa Shirika la Kazi duniani (ILO) namba 189 unaohusu kundi la wafanyakazi wa ndani kupata haki zao za msingi katika kazi zao sambamba na kuwezesha kundi hilo kutambulika kisheria.

CHODAWU
Pia serikali imeshauriwa endapo ikiridhia mkataba huo kutasaidia kundi hilo kuchangia uchumi wa nchi kwa namna moja ama nyingine.

Akizungumza jijini hapa jana wakati wa mkutano uliowakutanisha chama cha wafanyakazi wa hifadhi, mahoteli, majumbani, huduma za jamii na ushauri (CHODAWU), Katibu mkuu wa chama hicho, Said Wamba, alisema ni muhimu sasa serikali kuridhia mkataba 189 wa ILO ambao unaelekeza wafanyakazi wa ndani kupata haki zao za msingi.
"Ikumbukwe kuwa tarehe15 Juni mwaka jana kwenye kikao cha 100 cha ILO huko Geniva, Mh Dr Jakaya kikwete rais mstaafu alihutubia baraza hilo yaani nchi mwanachama ambapo miongoni mwa mambo aliyoyahutubia ni kuhusu suala la wafanyakazi wa majumbani huku akikiri kuwa Tanzania inawatambua wafanyakazi wa majumbani katika sheria za kazi sio tatizo,

"Na tarehe 16 Juni mkataba kuhusu Kazi za Staha kwa wafanyakazi wa majumbani ulipitishwa katika kikao cha ILO Geneva, na tunakumbuka Tanzania iliwakilishwa na Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) na waajiri ambao walipiga kura ya ndio na hivyo kupitishwa kwa mkataba wa ILO wa 189 na mapendekezo namba 201" alisema.

Aidha alisema endapo mkataba huo namba 189 utaridhiwa na serikali kutasaidia kuwepo kwa ajira zenye staha hususani kwa wanawake hali ambayo itapunguza umasikini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyakazi majumbani mkoa wa Dar es salaam, Marry Mwarabu, alisema kuwa kuridhiwa kwa mkataba huo kutasaidia kupatikana kwa mikataba yenye tija dhidi ya mishahara yao, sambamba na kuondoa majina ambayo yamekuwa yakitumika kwa lengo la kudhalilisha kundi hilo kama kuitwa Beki tatu.

"Sisi wafanyakazi wa majumbani hapa Tanzania tupo zaidi ya 1,728,228 kwa mujibu uliofanywa na ILO mwaka 2013 ambapo wengi wetu ni wanawake kuanzia umri wa 15-24, tunafanya kazi nyingi sana za majumbani lakini baadhi yetu tumekuwa tukitukanwa na waajiriwa wetu, kufanyiwa vitendo vya kikatili, na kudhalilishwa lakini kama mkataba huo ukiridhiriwa tunaamini tutatambulika na kupewa mishahara yetu kulingana na mkataba unavyoainisha" alisema.

Akizungumzia upande wa wafanyakazi wa ndani wanaokimbilia kufanyakazi mataifa ya Nje, Mwenyekiti huyo alisema ni kutokana na mishahara ya baadhi ya waajiri kutoridhisha nchini huku kwa upande wa mataifa ya nje kuwa na changamoto ya kuajiri mfanyakazi kwa mikataba isiyokuwa na maelezo ya kina.

Hata hivyo kwa upande wake Mratibu wa kukuza kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa majumbani kutoka ILO, Rehema Shija, alisema kwa mujibu wa tafiti muhimu zilozofanyika ndani na Nje ya nchi zinaonyesha nchi 22 pekee ndio zilizoridhia mkataba huo huku kwa upande wa bara la Afrika kuonekana ni nchi mbili pekee ambazo ni afrika kusini na Mauritius.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top