AUDIO: HANSCANA AELEZA CHANZO CHA AJALI WALIYOIPATA NA MSANII DARASSA

Lindiyetu.com imemkamata mmoja wa walionusurika na ajali iliyotokea jana mida flani hivi ya mchana iliyowahusisha rapper Darassa, Mr VS, producer Abbah pamoja na Hanscana.
Hanscana
Ni Hanscana ambaye alivutiwa waya na kuweza kutusanua mchongo mzima jinsi ajali hiyo ilivyotokea na kudai kuwa walishindwa kuelewa chanzo cha ajali hiyo ni nini.

“Kusema kweli chanzo cha ajali tunashindwa kukielewa, sisi wote wanne tumeshindwa kuelewa kwasababu Darassa ndio ambaye alikuwa anaendesha, njiani bila sababu yoyote gari ikaanza kubinuka chini juu kisha ikaanza kubiringita takriban mara 4 kisha ikagonga kibao ambacho kilikuwa pembezoni kisha ikasimama kuelekea kule ambako tumetoka, bahati nziru kwakuwa wote tulikuwa tumevaa mikanda wote tukatoka tukiwa salama.” Aliongea Hanscana.

Kiutamu zaidi unaweza kuisikiliza story hiyo full ikisimuliwa na Hanscana baada ya kuplay hii video hapa chini.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post