Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA MKOA WA LINDI AKERWA NA WATENDAJI KUTOWAJIBIKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndg  Godfery Zambi  akizungumza na wananchi wa Rushungi wilaya Kilwa kulia Mkuu wa wilaya Kilwa Christopher Ngub...
Godfery Zambi
Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndg Godfery Zambi akizungumza na wananchi wa Rushungi wilaya Kilwa kulia Mkuu wa wilaya Kilwa Christopher Ngubiagai.
zahanati ya Rushungi
Hali halisi ya jengo la zahanati ya Rushungi wilayani Kilwa Lindi.
zahanati ya Rushungi
Hichi ndio chumba cha uzazi zahanati ya Rushungi Wilaya ya Kilwa.

Na. Mwandishi Wetu, Kilwa
Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfery Zambi ametoa muda wa miezi mitatu kwa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wanawatembelea wananchi vijijini na kutatua kero zilizopo ikiwemo ya ushauri wa kilimo na mifugo.

Agizo hilo amelitoa baada ya wananchi kumlalamikia wakati wa mikutano yake aliyoifanya kwa nyakati tofauti akiwa katika ziara yake ya kuhimiza shughuli za maendeleo wilayani humo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Rushungi Mohamedi Omary alisema katika kijiji hicho kuna kero nyingi ikiwemo watendaji wa idara ya kilimo kutotembelea kutoa ushauri wakati wa kuandaa mashamba na kupanda na ukosefu wa huduma bora kwenye zahanati ya kijiji.

Akipokea kero hizo mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakuu wa vitengo kutoa ufafanuzi juu ya baadhi ya malalamiko yaliyotajwa, na kubaini kuwa wapo watendaji wasiyotekeleza wajibu wao ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kutofika kwa jamii, kufanya mikutano itakayoelimisha na kupatiwa njia sahihi ya kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.

Katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa amezindua rasmi barabara yenye urefu wa kilometa 22 iliyojengwa na kampuni ya statoil kwa garama ya shiling Billion 7.9 ambayo itaondoa adha kwa wananchi wa vijiji vya kiswere na Rushungi wilayani kilwa.

**************************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top