BAADA YA GARI LAKE KUUA SUGU AOMBA RADHI

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu jana aliwaomba radhi wakazi wa Mbeya, wanafamilia, ndugu wa marehemu Recho Lutumo (14) aliyefariki dunia baada ya kugongwa na gari lake juzi.Joseph Mbilinyi
Ajali hiyo ilitokea wakati gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Gabriel Andrew (43), mbunge huyo akiwamo lilipokuwa likitoka jijini hapa kwenda Uwanja wa Ndege Songwe (Sia).

Recho ambaye ni yatima na aliyekuwa akilelewa na bibi yake Neema Lutumo, aligongwa wakati akivuka kwenye alama za watembea kwa miguu eneo la Iyunga katika barabara kuu ya Zambia.

Sugu akiwa na baadhi ya viongozi wa Chadema jijini Mbeya alishiriki maandalizi na shughuli zote za mazishi ya mtoto huyo kuanzia nyumbani ambako ndiko alikoomba radhi.

******************

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post