Unknown Unknown Author
Title: YANGA SC YAKUBALI KICHAPO MJINI MBEYA DHIDI YA MBEYA CITY
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Yanga SC , leo November 2 2016 walishuka katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza dhidi ya ...
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Yanga SC, leo November 2 2016 walishuka katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza dhidi ya wenyeji wao Mbeya City katika mchezo wao wa 13 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017.
Mbeya City Vs Yanga SC
Yanga wakiwa ugenini huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo chao cha kwanza kutoka Stand United cha goli 1-0 September 25 2016, leo November 2 2016 wamekubali kipigo cha pili kutoka kwa Mbeya City wakiwa katika dimba la Sokoine Mbeya.

Mbeya City wamefanikiwa kuifunga Yanga goli 2-1, magoli ambayo yalifungwa na Mwasapili dakika ya 6 na Kenny dakika 36 goli ambalo lilichukua muda kidogo refa kufanya maamuzi kutokana na wachezaji wa Yanga kuligomea, Donald Ngoma ndio alifunga goli la kufutia machozi la Yanga dakika 4 za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko.


Hadi dakika tisini za mchezo zinamalizika matokeo yalibakia kuwa 2-1.

MSIMAMO WA LIGI YA VODACOM BAADA YA MICHEZO YA LEO.
VPL Standings

VPL top Scorers
**********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top