Unknown Unknown Author
Title: MISS TANZANIA ALIA KUTELEKEZWA NA KAMATI YA MASHINDANO HAYO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Miss Tanzania 2016 Diana Edward ambaye ndiye mrembo anayetarajiwa kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia ‘Mis...
Miss Tanzania 2016 Diana Edward ambaye ndiye mrembo anayetarajiwa kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia ‘Miss World’, ameilalamikia kamati ya mashindano hayo kwa kumtelekeza.
Diana Edward
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Diana ambaye kwa sasa anatakiwa awe kwenye maandalizi ya mashindano ya Miss World, amesem abado hajapata msaada wowote kutoka katika Kamati ya Miss Tanzania na serikali, ikiwa zimebaki siku chache kuweza kufikia kwenye mashindano hayo ya dunia.

Amesema kuwa kwa sasa yeye anachohitaji kwa sasa ni suport pamoja na msaada mkubwa kutoka kwa serikali, kwani yeye binafsi anajitahidi kufanya pale anapoweza.

“Tanzania, viongozi, serikai, Miss Tanzania cometee, i need suport, i need what i deserve, unajua mimi ni mtu ambaye najiongeza, kwa hiyo nikipewa suport kidogo i push it up, kuna watu ambao nimewaomba suport wamenipa vya kutosha, kwa hiyo i need what i deserve”, alisema Diana.

Kwa upande wa msemaji wa Kamati ya Miss Tanzania ameruka kuhusika na suala hilo.

Chanzo: eatv.tv

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top