Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwa ke Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Oktoba 2016. Kushoto ni Mtakwimu, Philbert Mrema.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini.
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2016 umebaki kuwa ni asilimia 4.5 kama ilivyo mwezi Septemba 2016.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam.
"Hii inaamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2016 imekuwa sawa na kasi ya upandaji wa bei ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2016" alisema Minja.
Minja alisema fahirisi za bei zimeongeza hadi 103.17 mwezi Oktoba, 2016 kutoka 98.72 mwezi Oktoba 2015 ambapo mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Oktoba 2016 umebaki kuwa asilimia 6.0 kama ilivyokuwa mwezi Septemba 2016.
Alisema mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba umechangiwa na kuongezeka kwa kasi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizi za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2015.
Akizungumzia uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 96 na senti 92 mwezi Oktoba 2016 ikilinganishwa na shilingi 97 na senti 04 ilivyokuwa mwezi Septemba 2015.
Aidha akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki alisema nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.47 kutoka asilimia 6.34 mwezi Septemba 2016.
Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umepungua hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.2 mwezi Septemba 2016.
***********
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.