MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA AVIFUTIA USAJILI WA KUDUMU VYAMA HIVI....!!

Msajili wa vyama vya siasa Tanzania amevifutia Usajili wa kudumu vyama vifuatavyo baada ya zoezi la uhakiki kufanyika na kuona havikidhi CHAUSTA, APPT MAENDELEO NA JAHAZI ASILIA.
Jaji Mutungi
Jaji Mutungi amefikia uamuzi huo kutokana kuwa vyama hivyo vimekuwa na ofisi upande mmoja jambo ambalo ni kinyume na kifungu 10d ambacho kinakitaka chama cha siasa kuwa na ofisi pande mbili kwa maana ya Tanzania Bara na Zanzibar.


Lakini sasabu ya pili ni kutokuwa na wanachama Zanzibar kwa mujibu wa kifungu 10b pia kushindwa kuweka wazi mapato na matumzi ya fedha za chama kama kifungu cha 14 (1) (a) kinavyoelekeza.
Source: JF

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post