Unknown Unknown Author
Title: LADY JAYDEE AMJIBU HIVI RUGE MUTAHABA KUHUSU KAZI ZAKE ZA MUZIKI (+AUDIO)
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Lady Jaydee amesema kauli aliyoitoa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group , Ruge Mutahaba kuhusu kuwa tayari kucheza nyimbo zake a...
Lady Jaydee amesema kauli aliyoitoa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kuhusu kuwa tayari kucheza nyimbo zake akiwaruhusu, ni sahihi na ya kiutuzima.
Lady Jaydee
Muimbaji huyo mkongwe ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano na mtangazaji wa Nyemo FM, ya Dodoma, Winston Makangale.

“Nimeisikia kauli ya Ruge, kwa namna aliyoiongea na nafasi aliyokuwa nayo, sioni kama kuna kitu kibaya chochote alichokifanya kwa jinsi ambavyo amezungumza, naona amezungumza sahihi tu,” alisema.

Amesema yeye na Ruge hawajahi kuzungumza kwa miaka minne sasa.

“Hajanipigia simu na wala sijampigia simu, kwahiyo sio kwamba tumeongea kitu chochote lakini nayaona tu ni maamuzi ya kikubwa ambayo yamefanyika hapo. Hatujaongea kwasababu tulikuwa na mgogoro,” ameongeza.

Jaydee amesema uongozi wake ndio utakaokuja na maamuzi kufuatia ofa ya Ruge.

“Kama kuna kauli yoyote ambayo itatakiwa kutoka, management itatoa kauli hiyo ya nini kitafuata.”


HII NI FULL INTERVIEW YAKE BOFYA PLAY KUSIKILIZA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top