Unknown Unknown Author
Title: WAGONJWA KUTOKA NNJE YA NCHI WAJA NCHINI KUTIBIWA MOYO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Matunda ya taasisi ya moyo ya JAKAYA KIKWETE yanazidi kuonekana baada ya wagonjwa mbalimbali kutoka nje ya nchi kufika katika taasisi hiyo ...
Matunda ya taasisi ya moyo ya JAKAYA KIKWETE yanazidi kuonekana baada ya wagonjwa mbalimbali kutoka nje ya nchi kufika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Taasisi ya Jakaya Kikwete
Wakizungumza katika tasisi hiyo baadhi ya wagonjwa wamesema taasisi hiyo inatoa huduma bora na zenye kuridhisha sawa na hospitali nyingine nje ya AFRIKA.

Katika siku ya pili ya upasuaji kwa watoto zaidi ya 50 wenye matatizo ya moyo kwa ushirikiano wa madaktari toka MAREKANI na TANZANIA, watoto watano wanatoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na UGANDA kama anavyoelezea mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Prof: MOHAMED JANABI.

Kiongozi wa watoto waliotoka nchini UGANDA JOHN FRANCIS ameeleza kuridhishwa kwake na huduma walizopata watoto aliokuja nao.

Baadhi ya mashirika yameanza kujitolea kugharamia za matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo likiwemo shirika la BAPPS CHARITIES TANZANIA ambao wametoa shilingi Milioni 220 kugharamia matibabu kwa watoto 100.

Tayari watoto SITA wamefanyiwa upasuaji mkubwa katika siku mbili tangu kuanza kwa zoezi la upasuaji litakalodumu hadi SEPTEMBA 19.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top