ZARI THE BOSSLADY ATEMA CHECHE KWA WABAYA WAKE, ANENA HAYA

Ni muda mrefu mahusiano ya Diamond na Zari yameelezwa kutokuwa mazuri kutokana na muimbaji huyo kuhusishwa kutoka na warembo wengine.
Zari
Kuna tetesi nyingi sana zimevuma kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni zikiwahusu Diamond na Zari.

Huku tetesi hizo zikimhusisha Diamond kusaliti mahusiano yake kwa kutoka na warembo wengine akiwemo Hamisa Mobetto na mrembo aliyetumika kwenye video ya wimbo wa ‘Kwetu’, Irene.

Kupitia mtandao wa instagram wa Zari ameandika ujumbe unaoonekana kuwalenga watu wanaomfuatilia na wasioyatakia mema mahusiano yao. “When your self made, it’s hard to break you no matter how hard they may try. I made me and the only person that can break me is ME not anybody. Ladies now wear this crown and put them heels on and keep it moving. Good night,” ameandika Zari.
Post
Hata hivyo wawili hao wanatarajia kupata mtoto pili wa kiume muda wowote kuanzia mwezi Disemba mwaka huu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post