ZAMARADI MKETEMA AJA NA FILAMU HII HAPA BAADA YA KUNG'ARA KWA FILAMU YA KIGODORO

Zamaradi Mketema amesema yupo mbioni kuachia filamu mpya ambayo anasema itakuwa gumzo.
Zamaradi Mketema
Akiongea na Bongo5, Zamaradi amesema filamu hiyo itakuwa tofauti na kwamba awali alipanga aiite Mchepuko lakini amebadilisha jina baada ya kuwepo nyingine yenye jina hilo.

Amesema bado ni mapema kusema itaitwaje lakini amedai kuwa ni tofauti kabisa na Kigodoro, filamu iliyompa tuzo. “Tumetoka kwenye upande wa Kigodoro kabisa tuko sehemu nyingine tofauti kabisa,” amesisitiza.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post