TCRA YASHUSHA RUNGU KWA ITV na CLOUDS MEDIA, YAWATOZA FAINI YA TSH 19 MILIONI KWA MAKOSA HAYA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kitengo chake cha maudhui Jumanne hii kimevitoza faini ya jumla TSh 19m vituo vya utangazaji, ITV, Clouds TV na Clouds FM kwa kukiuka kanuni za utangazaji.
TCRA
TCRA wanasema Clouds Media imepigwa faini hiyo kutokana na kosa la kushabikia mapenzi ya mbuzi na binadamu kwenye chombo chao cha habari na kupiga wimbo wa mwanamuziki Mwana FA ambao unapaswa kupigwa muda maalumu ambao wameagizwa.

ITV wamepigwa faini hiyo kutokana na kipindi kutoka bungeni kilichokuwa kinaoongozwa moja kwa moja, ambapo Mbunge wa Iringa Mjini alisikika akisema “Naibu Spika amekuwa kama anavaa pampas,hataki kubanduka kwenye kiti kuongoza bunge”.

TCRA
imewakumbusha wadau wote kufuata sheria na maadili ya utangazaji ili kuepuka adhabu na ukiukwaji wa maadili.

Source: Mwananchi/Jamii Forum

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post