Na. Fungwa Kilozo, Lindi
Nusu fainali ya Kwanza ya Mashindano ya RPC - CUP 2016 yanayofanyika katika Mji wa Lindi ndani ya kiwanja cha ILULU yameendelea leo hii na Kuzikutanisha timu za Mnazi Mmoja Vs Rasibura.Katika Mtanange huo ulioshuhudiwa na mashabiki lukuki kutoka katika kata mbalimbali zinazounda Manispaa ya Lindi na Kushuhudia Timu ya Rasibura ikitoa kichapo cha Goli 1-0 dhidi ya Mnazi mmoja.
Mchezo huo ulianza kwa Tension kubwa kwa Timu zote mbili kwani Timu hizo hazijawahi kukutana kutokana na kuwa makundi tofauti na hivyo kuanza kwa kusomana kimchezo. Kitendo hicho kilichangia kutoonyesha soka la kuvutia kwa timu zote mbili.
Hadi Kipindi cha Kwanza kinaisha matokeo yalikuwa 0-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kushambuliana kwa zamu kwa timu zote mbili lakini ilikuwa na faida kwa upande wa Timu ya Rasibura kupitia kwa Mchezaji wake ambae aliingia kipindi cha pili na kufanikiwa kuibuka shujaa wa mechi hiyo Msafiri Kambwili kufunga goli pekee ambalo lilipeleka kilio kwa mashabiki wa Mnazi mmoja.

Kesho Utachezwa Mchezo wa Pili wa Nusu fainali ya Mashindano hayo ukizikutanisha Timu za Mingoyo Vs Makonde. Mchezo huo utaanza kuchezwa saa 10.00jioni, Ndani ya Uwanja wa Ilulu.
Tags
SPORTS NEWS