GIGY MONEY AWATAJA MASTAA 6 ALIOTOKA NAO KIMAPENZI, ALI NA ABDU KIBA WOTE NDANI YA LIST HII

Gigy Money Jumanne hii aliwaacha mdomo wazi mashabiki wake baada ya kuwataja live kwenye runinga mastaa 6 wakiume aliotoka nao kimapenzi.
Gigy Money
Video queen huyo ambaye amewai kutamba katika video za mastaa mbalimbali wa bongo, amedai amewai kutoka kimapenzi na AliKiba, Abdu Kiba, Rich Mavoko, Harmonize, Hemed Phd pamoja na mtangazaji wa kipindi cha runinga cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Castro Dickson ambaye alidai alikuwa tayari kumzalia mtoto.
Rich Mavoko, Gigy Money and Hemed Phd
“Nilikuwa na Castro mpaka nilikuwa tayari kumzalia,” 
Gigy Money alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV. 
“Kwa sababu anajua upendo kwa mtoto, lakini wakaja wanawake wamjini wakakorofisha, lakini hajawai kuniambia kama tumeachana, sijui kama tumeachana,”
Gigy ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM alidai Mama yake mzazi alimzaa nyuma ya mlango wa choo.

Pia alisema kwamba aliwahi kujitoa kimwili katika umri mdogo ili apate hela ya kuweza kumnusuru mama yake mzazi kulipa deni la mkopo wa Benki.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post