Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku mbili baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania Mh. Nape Nnauye kutembelea maduka ya kazi za sanaa katika soko la Kariakoo jijini Dar es salaam na kubaini wauzaji wa kazi feki za sanaa.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam mkurugenzi wa kampuni hiyo Alex Msama amesema kuwa suala hilo ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono ukomeshwaji wa wahujumu uchumi na wakwepa kodi nchini Tanzania.
Aidha Msama amempongeza waziri Nape na kusema kuwa ni vyema watanzania wakafahamu kuwa kinachohitajika sasa ni watu kufanya kazi halali na sio kuwaibia wengine kwa njia tofauti tofauti.
Msikilize hapa chini akielezea.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.