Usiku wa kuamkia tarehe 10/7/2016 umekuwa ni wamajonzi kwa wakazi wa Lindi na Vitongoji vyake kwa kutokea kwa tukio la Kuungua Moto Shule ya Sekondari ya Lindi.
Mashuhuda wa Ajali hiyo wameeleza kuwa wanahisi chanzo cha ajali hiyo ni Hitilafu ya umeme.
Kikosi cha zimamoto kimelaumiwa na wadau mbali mbali kushindwa kutoa msaada wenyetija katika ajali hiyo na kusababisha Uharibifu huo kuwa mkubwa kwani gari la Zimamoto liliwahi kufika eneo la tukio lakini likishindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwani Mota ya kusukuma maji haikuwa ikifanya kazi hadi Kulazimu kutumia Gali za washa washa kusaidia kuzima moto huo.
Moto huo umeweza Kuathiri Madarsa Tisa, Ofisi nne, Matundu ya Vyoo 24, Maabara Mbili pamoja na Chumba cha kufanyia Midahalo.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ilifika eneo la tukio na kujionea uharibifu huo uliosababishwa na Moto huo.
TAZAMA VIDEO HII HAPA USHUHUDIE UHARIBIFU ULIOTOKEA
TAZAMA VIDEO HII HAPA USHUHUDIE UHARIBIFU ULIOTOKEA
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.