SAID FELLA AISAPOTI KIAINA DISS YA ROMA KWA BABU TALE, HICHI NDICHO ALICHOKISEMA

Lisemwalo lipo. Said Fella amedai kuwa mstari aliorap Roma kwenye wimbo wake ‘Kaa Tayari’ ni maneno hata mtaani yapo yanazungumzwa kila siku.
Said Fella
Add caption
“Bosi kamganda Dangote kaisahau Tip Top,” – amerap Roma kwenye wimbo huo.

Fella amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa mstari aliorap Roma ndani ya wimbo huo una ukweli ndani yake.
Said Fella na Bab Tale
“Unajua Roma ni mtu mzima, alichoimba hata mtaani huko watu wanasema, na unaweza kuona labda Roma ameambiwa hayo maneno na msanii kama Madee au msanii mwingine yeyote wa kwetu. Lakini hata mimi nilishawahi kumwambia mdogo wangu Babu Tale kuwa tufanye yote lakini yeye asiisahau Tip Top Connection na mimi nisiisahau TMK,” amesema Fella.
Said Fella na Bab Tale
Bado Tale hajajibu chochote kuhusiana na maneno hayo. Pamoja na kuwa meneja wa Tip Top, meneja huyo staa amekuwa akifanya kazi na Diamond na WCB nzima.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post