Timu ya Kata ya Mnazi Mmoja imeifunga timu ya Kata ya Mbanja kwa jumla ya magoli 2-0 katika Mashindano ya RPC - CUP yanayoendelea katika Uwanja wa Ilulu ndani ya Manispaa ya Lindi.
Ni Abdallah Ismail a.k.a Baloteli ndiye aliyeibuka Shujaa wa Mchezo huo baada ya Kuifungia Timu yake ya Mnazi mmoja magoli yote mawili ambayo yalipatikana katika dakika ya 38 na 50 ya Mchezo huo.
Hata hivyo Timu hiyo ya Mnazi mmoja walionekana kuidhibiti vilivyo wapinzani wao na kama safu ya Ushambuliaji ingekuwa makini ingeweza kuibuka na ushindi mmnono wa Magoli mengi zaidi.
Mnamo dakika ya 48 Timu ya Kata ya Mbanja waliweza kumpoteza Beki wao ambaye alivalia jezi namba 10 baada ya Kuzawadiwa kadi nyekundu mara baada ya Kuunawa Mpira kwa makusudi pale alipokuwa akitorokwa na Mshambuliaji Machachari wa Timu pinzani.
Hadi Mwisho wa Mchezo Mnazi mmoja waliibuka washindi wa Mechi hiyo kwa Jumla ya magoli 2-0.
Hadi Mwisho wa Mchezo Mnazi mmoja waliibuka washindi wa Mechi hiyo kwa Jumla ya magoli 2-0.
KIKOSI CHA KWANZA CHA TIMU YA KATA YA MMNAZI MMOJA DHIDI YA KATA YA MBANJA
KIKOSI CHA KWANZA CHA TIMU YA KATA YA MBANJA DHIDI YA KATA YA MMNAZI MMOJA
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.