SHIRIKA la Kuendeleza Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoani Lindi, limewapatia wajasiliamali 49 mkopo wa thamani ya Sh. milioni 58, kwa lengo la kuinua na kuboresha mitaji ya biashara zao.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Yahya Nawanda, alikabidhi hundi za mikopo hiyo, katika ofisi za SIDO mjini hapa.
Akitoa maelezo mafupi, Ofisa Mikopo wa SIDO Mkoa wa Lindi, Salma Ally, alisema huo ni mkopo wa pili kutolewa kwa mwaka huu kwa wajasiliamali wa wilaya hiyo.
Salma ambaye pia ni Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Lindi, alisema kati ya fedha hizo, Sh. Milioni 15 zimetolewa kwa vikundi vitano vinavyojishughulisha na kazi mbalimbali.
Alivitaja vikundi hivyo kuwa ni vya mafundi uchomereaji vyuma, ushonaji, mama lishe, ufugaji, uzalishaji chumvi, utengenezaji matofali na watu binafsi.
Akizungumza baada ya kukabidhi hundi hizo, Nawanda aliwataka kutumia mikopo wanayochukua kwa kuifanyia kazi iliyokusudiwa, ili kuwaondoa kwenye lindi la umasikini na kuwa na maisha bora.
Nawanda pia aliwataka wajasiliamali hao kuwa waaminifu na fedha hizo, ikiwamo kurejesha kwa wakati mikopo wanayoichukua, ili kusaidia na wengine.
“Serikali inapenda kuona hii mikopo mnayoichukua inaleta tija kwenu na kwa serikali pia, kutokana na kodi mtazokuwa mnalizilipia,” alisema Nwanda.
Baadhi ya wajasiliamali walionufaika na mikopo hiyo, Iddi Toto na Zuhura Ismaili, kwa nyakati tafauti waliishukuru SIDO kwa kuwajali wajasiliamali katika kuwapatia mikopo ambayo inawasaidia kuinua mitaji yao.
Hii ni mara ya pili kwa SIDO mkoani Lindi kutoa mikopo. Machi, mwaka huu, wajasiliamali 49 walipatiwa mikopo ya zaidi ya Sh. Milioni 49.