HARMONIZE AMTAMBULISHA WOLPER UKWENI, TAZAMA PICHA HAPA (+Picha)

You know it’s real pale unapompeleka ukweni mchumba wako na kumtambulisha kwa baba na mama.
Wolper and Harmonize
Wikiendi iliyopita hitmaker wa Bado, Harmonize alimpeleka mpenzi wake Jacqueline Wolper kwao Mtwara alikoenda kutumbuiza kwa mara ya kwanza tangu aukwae ustaa kupitia label ya WCB.
Wolper
“Time Ya Kumsaidia mama Harmo Kuanda Chakula Cha Usiku Mtwara Life @wolperstylish,” aliandika Harmonize kwenye picha inayomuonesha Wolper akichuma matembele shambani.

Naye Wolper alipost picha akiwa na mama mkwe na kuandika: I am having the best time of my life.. Nikiwa na Mama angu… Kabla hamjatoka lazima mpige story, akuchekeshe… Mjipikilishe.. Akushauri
Hapa nimepata rafiki kwa kweli…I love my mama Mkwe.. Mama Raj wangu.”
Wolper
Kwenye picha nyingine akiwa na mpenzi wake hiyo, Wolper aliandika:
"Pale unapotoka kula ugali wa muhogo na sangara kwa mkwe yani ni amani tu…dizaini na ka rangi kamezidi kukubali.”

Uhusiano wa mastaa hao wawili umetengeneza vichwa vya habari mwezi huu baada ya kuamua kuuweka wazi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post