WENGER KIMENUKA..!! MASHABIKI WAMPA MECHI MOJA TU, AKIFUNGWA ASEPE.

MASHABIKI wa Arsenal sasa wamechoka na kwamba wamempa kocha wao, Arsene Wenger mechi moja tu, akifungwa tena, afungashe virago.
Mashabiki wa Arsenal
Ripoti ya gazeti la Daily Express inadai kwamba Wenger amepewa mechi moja ya marudiano dhidi ya Hull City kwenye Kombe la FA kesho Jumanne, akifungwa, basi abwage manyanga, asepe.

Mashabiki wa timu hiyo ambao kwa muda mrefu hawajafurahia timu yao ikipata ushindi wanadhani kama watafungwa na Hull City kwenye mchezo huo basi hakutakuwa na haja ya Mfaransa huyo kuendelea kuwa kocha wa Arsenal msimu ujao.

Uamuzi wa kocha Wenger ang’oke kwenye timu hiyo ulipamba moto baada ya Arsenal kuchapwa na Swansea City kwenye Ligi Kuu England wiki iliyopita ambapo kilikuwa kipigo cha tatu mfululizo kwa timu hiyo.
Arsene Wenger
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ilidai kwamba malalamiko ya mashabiki wa timu hiyo ambao kwa muda mwingi wamekuwa watulivu yameanza kuwagusa wakurugenzi na huenda wakamtimua kocha huyo.

Arsenal juzi Jumamosi ilishindwa kupata ushindi baada ya kumalizisha sare ya mabao 2-2 na Tottenham kwenye Ligi Kuu England na hivyo kuachwa na vinara Leicester City kwa tofauti ya pointi nane.
Previous Post Next Post