Wakazi wa Kijiji cha Likong'o Kata ya Mbanja Manispaa ya Lindi wanakabiliwa na Changamoto ya Upatikanaji wa Huduma za Afya.
Wakizungumza na Lindiyetu.com wamesa kuwa maisha yao yako Hatarini kutokana na kituo cha Afya kuwepo Mbali na Makazi yao hivyo kupelekea hali ya wasi wasi mkubwa kwa wakinamama wajawazito hasa nyakati za usiku pale wanapohitaji huduma za Afya.
Mkazi mmoja wa kijiji hicho amesema kuwa wanatembea umbali wa Km 7 kufuata huduma za Afya.
Mama mmoja ambaye hakupenda jinalake kutajwa Mtandaoni amesema kuwa wanapata tabu hasa kutokana na gharama kubwa za ukodishaji wa Usafiri aina ya Boda Boda kwani ndio njia pekee waliyonayo ya kumfikisha mgonjwa nyakati za usiku.

UNAWEZA KUWASIKILIZA KWA KUBOFYA PLAY