TAZAMA VIDEO YA GOLI LA SAMATTA DHIDI YA CHAD ILIYOIPA USHINDI STARS UGENINI

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 ilikuwa katika uwanja wa Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017.
Mbwana Samatta
Mbwana Samatta ambaye amevaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza, amefunga goli hilo kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Farid Musa goli ambalo limedumu hadi dakika 90 za mchezo huo.
Mbwana Samatta
Stars hadi sasa imefikisha pointi 4 baada ya kucheza michezo 3, matokeo hayo yanaifanya Stars ifikishe pointi sawa na Nigeria ‘The Super Eagles’ lakini Stars ipo mbele ya Nigeria kwa mchezo mmoja. Nigeria itakutana na Misri kwenye mchezo wa kundi ilo siku ya Ijumaa.


Stars itacheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Chad siku ya Jumatatu March 28 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Previous Post Next Post