RICH MAVOKO SASA RASMI NDANI YA LABEL YA "WCB" YA "SIMBAAA" DIAMOND PLATNUMZ

Mmoja kati ya member wa ‘label’ ya WCB, Harmonize amethibitisha kuwa Rich Mavoko ni mmoja kati ya wasanii wa label hiyo.
Rich Mavoko na Diamond
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatano hii, Harmonize alisema label ya WCB ina wasanii watatu yeye mwenyewe , Raymond aliyekuwa Tip Top Connection pamoja na Rich Mavoko.
“Unajua mwanzo zilikuwa ni tetesi lakini naweza kusema ‘its official’ sasa Rich Mavoko yupo chini ya WCB,” alisema Harmonize

Aliongoza, “Kusema kuwa Rich Mavoko amenyoosha mikono kwa Diamond si vizuri kwani watu wanaweza kupata picha tofauti maana si unajua watu wanaweza kupokea jambo kwa maana na ikaleta picha mbaya wakati ni jambo la kawaida,”
Previous Post Next Post