Maombi yalifanyika kwake na mke wake ili Mungu amtangulie katika utumishi wake serikalini.
Mh. Paul Makonda alipokuwa akizungumza .
Mh. Paul Makonda akiwa na Mke wake akimshukuru Mungu
Akitimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni, asubuhi ya Jumapili ya jana, Paul Makonda katika Ibada Kanisani Living Water Center Ministry Kawe alipokelewa kiroho na kumshukuru Mungu kwa kutoa sadaka ya shukrani kwa hatua aliyofikia.
Katika Ibada hiyo Mhe. Makonda ambayo aliongozana na mkewe, alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema haikuwa raisi kwake ila Mungu amemuwezesha na kuwatia moyo, "Usishindwe kufanya mambo ya kimaendeleo kwa changamoto za kimazingira au chochote," akisema kama ambavyo imekuwa ikionekana kwake.
Mapema akimkaribisha kuzungumza, Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi alikuwa anaelezea jinsi ambavyo amemlea kiroho Mhe. Makonda hata kabla ya kuingia kuwa mtumishi wa serikali, jinsi alivyokuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali na hivyo kinachofanyika leo sio kipya kwake na Bwana akatenda zaidi kwa kumfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tags
HABARI ZA KITAIFA