Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Mkuu mpya wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amehaidi kuyavunja mabaraza ya ardhi ya kata atakayo yabaini yanatenda kazi zake kinyume cha taratibu na sheria.

Zambi ameyasema hayo wa mkutano na wazee wanaoishi katika Halmashauri za Manispaa na Wilaya ya Lindi, uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo.
Alisema miongoni mwa kero ambazo wanalalamikia wananchi, hasa wanyonge ni baadhi ya mabaraza ya ardhi kutuhumiwa kwa rushwa.
Alisema ni jambo lisilokubalika kuona waliopewa dhamana ya kuwaongoza na kuwahudumia wananchi wanakuwa ni sehemu ya kero.
"Kwamamlaka niliyonayo kisheria ninauwezo wa kuyavunja mabaraza ya ardhi ya kata, kwahiyo tukichunguza na kubaini kama kunabaraza yanatenda ndivyo sivyo nitalivunja," alisema Zambi.
Kwa upande wa mabara ya Wilaya, Mkuu huyo wa Mkoa alisema yatayobainika kwenda kinyume cha taratibu na sheria, ikiwamo vitendo vya rushwa atapeleka taarifa kwa waziri mwenye dhamana ya sheria awezekuchukua hatua baada ya kushauriana na mwanasheria mkuu wa serikali.
"Nisingependa kusikia wala kuona migogoro ya ardhi katika mkoa huu,wazee tusaidieni tutakapo kuwa tunachukua hatua,kwani tutakayoyafanya nikwafaida ya wananchi," aliongeza kusema.
Aidha Zambi alitoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa ambao pia walikuwepo kwenye mkutano huo,washirikiane na kujiona ni ndugu.
Huku akivifananisha vyama kama njia tofauti wanazopitia viongozi hao, lakini lengo lao ni moja la kuwapelekea maendeleo wananchi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wazee wastahafu wa Lindi (CHAWALI), Abdallah Majumba alimuomba mkuu huyo wa mkoa kusimamia kwa karibu uanzishwaji wa mabaraza ya wazee ya vijiji na kata ili waweze kuwa na sauti ya pamoja.
Tags
HABARI ZA KITAIFA