Karibia kila chombo cha habari duniani sasa hivi kina ripoti ishu ya mlipuko wa mabomu ndani ya Airport huko Brussel Belgium leo asubui.

Mlipuko huo umetokea kwenye Airport kubwa ambapo wananchi wa mataifa mbalimbali wamejeruhiwa. Ripoti kamili hadi jioni hii ni kwama watu 28 wamepoteza maisha na wengine 12 wamejeruhiwa kwenye mfululizo wa milipuko ya mabomu uwanjani hapo.

Wakati mlipuko huo unatokea hapo uwanjani kulikua na striker wa club ya Norwich Dieumerci Mbokani ambae ni raia wa Congo akiwa kwenye safari. Baada ya mlipuko huo club yake ilifanya mawasiliano nae na walitoa statement kwamba Mbokani yupo salama na hajapata tatizo lolote licha ya kuwa ndani ya Airport hiyo.
Tags
SPORTS NEWS