HATIMAE LINAH AFUNGUKA KUMZIMIKIA WIZKID, AZUNGUMZIA SUALA LA KUTOKANAE WAKATI YUKO NCHINI NIGERIA

Msanii wa muziki Linah Sanga ameweka wazi kwamba anatamani kutoka kimapenzi na staa wa muziki kutoka Nigeria Wizkid.
Linah Sanga
Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Jumanne hii, Linah amesema mwanaume ambaye anawish kuwa naye ni Wizkid.
“Msanii gani wa Afrika wakiume ambaye ningependa kuwa na mahusiano naye ambaye nilikuwa nampenda au nawish kuwa naye ni Wizkid,” alisema Linah.
Linah Sanga
Pia Linah amedai hakupendezwa na tetesi ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa alilala na Wizkid wakati ambapo alikuwa Nigeria kwa ajili ya show.
Previous Post Next Post