WAFANYA BIASHARA WA MAZAO YA MISITU KANDA YA KUSINI WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO NA FURSA ZA ZILIZOPO KATIKA BIASHARA MISITU

Wakala wa Misitu(TFS)
Meneja wa Wakala wa Misitu(TFS)Kanda ya Kusini akitoa mada kuhusiana na Taratibu na sheria za Uvunaji wa mazao ya Misitu
Wakala wa Misitu(TFS)
Mshauri wa Kampeni ya Mama Misitu, Bw Cassian Sianga akipitia baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na wafanya biashara wa Mazao ya Misitu katika warsha inayoendela Mjini Lindi
Wakala wa Misitu(TFS)
Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wakiwa ktk mjadala wa pamoja mjini lindi

Na. Mwandishi Wetu, Lindi
Wafanyabiashara wa mbao na magogo kanda ya kusini wakutana mjini lindi kujadili fursa na changamoto za biashara ya mazao ya misitu ili kueneza shughuli za Usimamizi Shirikishi wa Misitu Nchini Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) pamoja na washirika wake; Shirika la Kuhifadhi Mpingo na Maendeleo-MCDI, Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania-MJUMITA, Shirika la WWF Tanzania pamoja na Kampeni ya Mama Misitu.

Lengo la Warsha hiyo ya wafanyabiashara ni pamoja na kuongeza nguvu katika jitihada za kuimarisha mijadala kwa wafanyabiashara wa mbao/magogo juu ya mambo muhimu yanayosibu biashara ya mazao ya misitu ikiwemo kuoanisha baadhi ya Changamoto na Mafanikio.

Warsha hiyo imelenga katika kuwasilisha fursa zilizopo za kufanya uvunaji katika misitu ya hifadhi za vijiji ikilinganishwa na uvunaji katika misitu ya wazi ikiwa pamoja na kutoa ufafanuzi wa mambo ya kitaalam yahusuyo upimaji na ukadiriaji wa ujazo wa mbao.

Sambamba na utekelezaji wa shughuli za mradi wa washirika WWF Tanzania na Jumuiko la Maliasili Tanzania unaohusu mambo ya uwekezaji katika misitu na ardhi (unaofadhiliwa na WWF Finland kupitia ofisi za WWF Tanzania) pamoja na shughuli za Kampeni ya Mama Misitu (inayofadhiliwa na Serikali ya Finland). Miradi hii miwili ndiyo itakayogharimia warsha hiyo.

Warsha Hiyo Imehusisha wafanyabiashara toka wilaya za Liwale, Tunduru, Masasi, Nachingwea, Ruangwa, Kilwa, Lindi na Rufiji.
Previous Post Next Post