NIJUZE NIJUZE Author
Title: CHADEMA WASHIKANA UCHAWI WILAYANI NACHINGWEA, LINDI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Na.Ahmad Mmow,Nachingwea.   Madonda yaliyosababishwa na uchaguzi mkuu uliopita, hayajapona na yanaendelea kukitesa Chama Cha Demokrasi...
Na.Ahmad Mmow,Nachingwea.  
Madonda yaliyosababishwa na uchaguzi mkuu uliopita, hayajapona na yanaendelea kukitesa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika wilaya hii ya Nachingwea.
UKAWA, Nachingwea
Katika hatua ya sasa katibu wa wilaya wa chama hicho aliyefukuzwa na kamati ya utendaji wa wilaya hiyo kwa tuhuma za kukisaliti wakati wakampeni za uchaguzi uliopita, Yassin Nakanyomwa, amewa tuhumu katibu wa idara ya  itikadi, uenezi na siasa, aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia chama hicho, Dkt Mahadhi Mmoto na kamati ya utendaji ya wilaya kwamba wanapanga safu mpya ya uongozi kwa misingi ya ukabila.

Nakanyomwa aliyasema hayo juzi, alipozungumza na Lindiyetu.com, mjini Nachingwea. Nakanyomwa ambaye anadai bado ni katibu wa wilaya hii na hatambui kuondolewa kwake, kwasababu kikao kilichomuondoa kilikuwa batili, kutokana na kutotimia akidi ya wajumbe.

Alisema tuhuma za kukisaliti chama wakati wa uchaguzi ni zakutungwa zenye lengo la kumuondoa kwenye nafasi hiyo ili waingizwe viongozi wapya ambao niwakabila ya kimakonde. Alisema lengo la mkakati huo ni maalumu kwa kumuandalia mazingira aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia chama hicho,Dkt Mmoto ambaye anashiriki mkakati huo, aweze kushinda kirahisi kwenye kura za maoni ndani ya chama mwaka 2020. ili awe mgombea wa ubunge wa jimbo la Nachingwea, ambalo sasa mbunge wake ni Hassan Masala wa Chama Cha Mapinduzi. 

Alizitaja  tuhuma anazotuhumiwa nazo ni pamoja na kuvujisha mipango na mikakati wakati wa uchaguzi. 

Tuhuma nyingine aliyoitaja nikushirikiana na mgombea wa ubunge wa CCM na kumpa mikakati inayopangwa na chama hicho."Wanasema hata TV( Runinga)ninazotumia kwenye biashara zangu nilipewa na aliyekuwa mgombea wa ubunge wa  CCM, pia kukodi banda la CCM kuendesha biashara zangu" wanasahau hata nilipochaguliwa kuwa katibu nilikuwa nafanyabiashara hizi kwenye banda hili," alisema Nakanyomwa.

Alikwenda mbali nakumtuhumu katibu wa mwenezi na siasa, Hamisi Majaliwa kuwa anasitahili kuitwa msaliti. Kwamadai kuwa aliwahamasisha baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mandai wasimpigie kura mgombea wa udiwani wa kata ya Mkotokuyana kupitia chama hicho, Ahmad Likolovela, ambaye aliangushwa na mgombea wa CCM, Saada Makota."Tena yeye alichukua kadi akawapa CCM wakati wa kampeni, na CCM wakawa wananadi kwenye mikutano yao kama kunawanachama wa CHADEMA walihama na kujiunga na CCM," aliongeza kusema Nakanyomwa.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya wilaya ambaye hakutaka jina lake kutajwa kwamadai sio msemaji wa chama hicho, alisema tuhuma alizozisema Nakanyomwa sio zilizosababisha aondolewe.

Bali kushindwa kufikisha maagizo ya makao makuu wakati wa uchaguzi. Lakini pia kuficha na kukumbatia vifaa wakati wa uchaguzi ikiwamo mabango ya picha ya mgombea wa uRais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa."Wakati wa kampeni wanachama na vingozi wa kata na matawi walikuwa wanaambiwa hakuna mabango, lakini baada ya uchaguzi aliyaleta na mengine yalionekana yamechanwa na yamezagaa hadi kwenye mitaro ya barabara" hiyo kama sio hujuma tuite kitugani na nani anaweza kuvumilia usaliti wa aina hiyo," alieleza na kuhoji mjumbe huyo wa kamati ya utendaji ya wilaya.

Kwa upande wake, Hamisi Majaliwa licha ya kupuuza tuhuma dhidi yake akiziita nizakizushi. Lakini pia alisema uamuzi  wa kamati ya utendaji ulikuwa halali kwasababu idadi ya wajumbe waliotakiwa kwa mujibu wa katiba walitimia. 

Akaongeza kusema kwenye kikao cha tathimini ya uchaguzi uliopita, aliachia ngazi mwenyewe baada yakushindwa kujitetea. 

Naye Dkt Mahadhi Mmoto, alisema hafikirii kupanga safu ya uongozi, kwa madai kuwa wenye uwezo wa kupanga safu ya uongozi ni wanachama kupitia vikao vilivyopo kwa mujibu wa katiba ya chama hicho. Bali mkazo wake mkubwa nikukijenga chama na kuongeza idadi ya wanachama.

Hata hivyo alitahadharisha kuwa mambo hayo yatafanikiwa iwapo chama kitakuwa na viongozi imara na makini. Kuhusu tuhuma za ukabila, alipuuza nakuziita porojo ambazo hazikuwa na nafasi ya kujadiliwa nakuzungumzwa na watu makini.

About Author

Advertisement

 
Top