NIJUZE NIJUZE Author
Title: #AfyaYako :: VIAZI VYEKUNDU (BEETROOTS) VINASAIDIA KUPUNGUZA SHINIKIZO LA DAMU
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Viazi vyekundu ambavyo hujulikana kama beetroots kwa kiingereza ni viazi vya mimea aina ya beets, huwa na rangi nyekundu vingine vikiwa nja...
Viazi vyekundu ambavyo hujulikana kama beetroots kwa kiingereza ni viazi vya mimea aina ya beets, huwa na rangi nyekundu vingine vikiwa njano au vyeupe.
Viazi vyekundu
Utafiti uliofanyika siku za karibuni katika Vyuo Vikuu vya Tiba vya Barts na London School of Medicine nchini Uingereza, umeonesha kuwa unywaji wa juisi yenye viazi vyekundu kila siku kwa watu wenye shinikizo la damu la kupanda husaidia kupanguza shinikizo la damu.

Viazi vyekundu vina madini ya nitrate ambayo husaidia kutanua na kulainisha mishipa ya damu, hivyo kupunguza shinikizo la damu na pia huimarisha kuta za ndani za mishipa ya damu.
Viazi vyekundu
Unaweza ukatumia viazi vyekundu kama juisi ya kusaga, au ukachanganya na matunda mengine kama maembe n.k.

Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya viazi vyekundu kila siku peke yake au zaidi ya glasi moja kila siku kama ukiwa umechanganya na matunda mengine.
Viazi vyekundu
Vina madini ya potasiamu, chuma, vitamini A, B6 na C, asidi ya foliki, protini na wanga.

About Author

Advertisement

 
Top