STAA wa filamu za Kibongo, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’, amefichua kuwa anatongozwa na zaidi ya wanawake wanane kwa siku, kutokana na umaarufu wake.
Akiongea na Saluti5, Gabo alisema kuwa, amekuwa akipata taabu kutokana na hilo, hasa kwa sababu ameelekeza zaidi fikra zake kwenye kazi na si mapenzi kama wao wanavyodhani.
“Nafikiri wanawake wengi wanavyoniona kwenye runinga wanaamini ndivyo nilivyo, huku kumbe nakuwa ‘Gabo’ ninapoigiza tu na nje ya hapo mimi ni ‘Salim Ahmed’ wa kawaida,” alisema Gabo.
Alisema, kwa upande wake hiyo ni kati ya changamoto kubwa anazokabiliana nazo, huku akiwataka wanawake hao waache kumtongoza kwa kumuona kwenye muvi akidai kuwa wanajidhalilisha bure sababu hana nia nao.
Source:: Saluti5