Mbwana Samatta.
Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
Kirahisi tu, Kasongo amesema Samatta ni lazima ajiunge na timu yenye uwezo wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa) au Kombe la Europa, ambako anaweza kukutana na Wayne Rooney wa Manchester United au Santi Cazorla wa Arsenal.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kasongo alisema mpaka sasa wana ofa kutoka timu za mataifa matano lakini jambo la msingi kwao ni kuangalia uwezekano wa kucheza katika klabu inayoshiriki michuano mikubwa Ulaya.
“Bado tupo katika mazungumzo kwa sababu ofa ambazo mpaka sasa tunazo mezani zinatoka katika nchi za Ujerumani, Ufaransa, Bulgaria, Hispania na Ubelgiji, ila ukiitoa Bulgaria, nchi zilizobaki anaweza kucheza".
“Hatuwezi kusema moja kwa moja kama anakwenda Ufaransa kwa sababu tunataka timu ambayo itacheza michuano hiyo ya Uefa na pia iliyo katika hali nzuri kwa masuala ya maslahi".
“Samatta akicheza Uefa au Europa atakuwa amefika mbali sana na atajitangaza yeye mwenyewe na Tanzania kwa jumla hivyo ni lazima tuliangalie hilo kwanza,” alisema Kasongo.
TP Mazembe ipo katika harakati za kumuuza straika Mbwana Samatta kwenda Lille ya Ufaransa, lakini meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kasongo ametoa sharti jipya la nyota huyo kwa timu atakayoenda.