Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya vyumba vitano vya madarasa vilivyojengwa kwa ustadi mkubwa na taifa la marekani kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 400 katika shule ya msingi Boma, mkuu wa wilaya ya mkinga Bibi Mboni Mgaza amesema utafiti uliofanywa umeonesha kuwa baadhi ya wanafunzi hao wamejifungua kwa sababu ya wazazi kushindwa kuhimiza elimu kwa watoto wao.
Awali akielezea lengo hasa la ujenzi wa vyumba vya madarasa, afisa uendeshaji wa kikosi hicho kamanda Davd Dickerson amewataka wananfunzi watumie vyema fursa hiyo kwa sababu taifa la marekani linataka kuhakikisha kuwa elimu katika nchi rafiki za afrika inaimarika ili kuleta maendeleo ili kupunguza adha ya wanafunzi.
Kufuatia hatua hiyo halmashauri ya wilaya ya mkinga kupitia mwalimu mkuu wa shule ya msingi boma bwana john msulwa wameshukuru kwa msaada huo kwa sababu wanafunzi zaidi ya 500 wanaosoma katika shule hiyo baadhi yao walikuwa wakisoma kwa kupeana zamu ya kuingia darasani kwa sababu ya upungufu wa vyumba vya madarasa.