Rapa kutoka Afrika Kusini, A.K.A ameshangazwa na ripoti kuwa ana mpango wa kumfungulia rapa wa kimataifa Drake mashtaka ya kudai fidia, akilalamikia star huyo kumuiga wazo la video na mtindo wa kudansi ambao ametumia katika video ya Hotline Bling.
A.K.A
Star huyo kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter amewaonyesha mashabiki wake kuwa anashangaa kukutana na taarifa kama hizo, hatua ambayo inadhihirisha kuwa si habari za ukweli, licha ya vyombo vingi kunukuu na kusambaza habari hiyo.
DRAKE
Vilevile star huyo ameweka wazi kuwa hafahamu chochote juu ya taarifa za mpango wa kufanya show ya kujaza uwanja mkubwa wa FNB huko Soweto ambao kampeni yake inaendelea kusambaa mitandaoni baada ya tukio la hasimu wake Casper Nyovest kufanikisha show yake iliyojaza uwanja mkubwa kama huo hivi karibuni.