Unknown Unknown Author
Title: NAY KUJA NA UJIO WA KITOFAUTI KABISA, MWENYEWE AZUNGUMZIA UJIO WAKE HUO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Msanii Ney wa Mitego amesema baada ya harakati za kampeni sasa yuko location kutengeneza video ya wimbo wake mpya ambao anatarajia kuuachia...
Msanii Ney wa Mitego amesema baada ya harakati za kampeni sasa yuko location kutengeneza video ya wimbo wake mpya ambao anatarajia kuuachia siku za hivi karibuni.
Ney wa Mitego
Ney wa Mitego ameiambia timu ya Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa utengenezaji wa video hiyo ulianza kabla ya kampeni, lakini alilazimika kusitisha kutokana na kampeni, na kwamba wimbo huo utakuwa na ladha tofauti na tulizozoea.
"Wimbo unaitwa nyumbani kwetu, ni muziki fulani hivi ambao sijawahi kufanya pia hii ni suprise kubwa sana kwa mashabiki wangu, na sidhani kama kuna mtu alishawahi kufikiria kuwa naweza nikafanya muziki wa dizain hii, so watu wakae tayari, tulishaanza kushoot kabla ya kampeni hazijaanza, lakini baada ya kuanza tulikuwa tumestop, so leo ndo tunamalizia, mpaka Jumatatu utakuwa tayari na Jumatano au ijumaa nitauachia", alisema Ney.

Kitendo hicho cha Ney kuachia nyimbo pamoja video pamoja ni mara ya kwanza kwake, kwani hajawahi kuachia wimbo pamoja na video.
"Sijawahi kuachia audio na video kwa pamoja, lakini nadhani hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza, kama haitoanza video basi itatoka audio na video kwa pamoja", alisema Ney wa Mitego alipokuwa akiongea na timu ya Planet Bongo.

About Author

Advertisement

 
Top