Ommy Dimpoz ameshinda tuzo ya African Entertainment Awards zilizofanyika Jumamosi hii huko New Jersey, Marekani.
Kufuatia ushindi huo, muimbaji huyo aliandika kwenye Instagram, “ Thank you my people for your Votes U made this Possible #PeopleChoiceAward @africanentertainmentawards #NewMusicComingSoon.”
Waandaji wa tuzo hizo hadi Jumapili walikuwa hawajatoa orodha nzima ya washindi.
Ommy Dimpoz, Mubenga na DMK wakiwa red carpet
Ommy aliyetumbuiza pia kwenye tuzo hizo alishinda kipengele cha People’s Choice Award.Kufuatia ushindi huo, muimbaji huyo aliandika kwenye Instagram, “ Thank you my people for your Votes U made this Possible #PeopleChoiceAward @africanentertainmentawards #NewMusicComingSoon.”
Waandaji wa tuzo hizo hadi Jumapili walikuwa hawajatoa orodha nzima ya washindi.
Katika hatua nyingine hitmaker huyo wa ‘Wanjera’ na muimbaji wa Uganda, Eddy Kenzo, wameingia studio kurekodi wimbo pamoja.
Ommy alishare kipande kifupi cha video kwenye Instagram kinachomuonesha Kenzo akiingia sauti za wimbo huo huku Ommy akisikika akimpa maelekezo kadhaa ya kuboresha vionjo vya wimbo huo.
Wawili hao walikutana Marekani walikoenda kuhudhuria tuzo hizo ambapo Eddy naye alishinda.