Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu wa mahakama ya Rufani Damian Lubuva.
TAARIFA KWA WAKAZI WA JIMBO LA MASASI
Hivyo basi kampeni rasmi za uchaguzi huo zitaanza tena tarehe 05/11/2015 na kumalizika tarehe12/12/2015 ambapo uchaguzi utafanyika tarehe 13/12/2015.
WAGOMBEA:
- RASHID CHUACHUA - CCM
- ISMAIL MAKOMBE (KUNDAMBANDA) - CUF
- DKT. PETER TIMOTHY OMARI - ACT-WAZALENDO
- MUSTAPHA SWALEHE - CHADEMA.
NB: Chama cha NLD kinafanya mazungumzo ya mwisho na uongozi wa UKAWA na pindi watakapokamilisha watatoa rasmi jina la Mgombea wao atakayeziba nafasi ya Marehemu Dkt. Emanuel Makaidi na tutawajulisha.
WITO:Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Masasi bado anawaomba wakazi wa jimbo la Masasi kuendelea kushiriki mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa kwa amani na utulivu kama ilivyokuwa hapo awali.