NIJUZE NIJUZE Author
Title: COLLABO YA WIZKID NA DIAMOND HAIEPUKIKI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Diamond Platnumz amefanya collabo na kila msanii mkubwa wa Nigeria. Ameshafanya ngoma au kushiriki kwenye ngoma na P-Square, Davido, D’Ban...
Diamond Platnumz amefanya collabo na kila msanii mkubwa wa Nigeria.Wizkid na Diamond Platnumz
Ameshafanya ngoma au kushiriki kwenye ngoma na P-Square, Davido, D’Banj, Tiwa Savage, Iyanya, Waje, Kcee, Bracket, Flavour na wengine lakini ni msanii mmoja tu mkubwa hajakutana naye kwenye wimbo wowote – Wizkid.

Wawili hao walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye show ya Leaders Club jijini Dar es Salaam, na picha zinaonesha kuwa tayari zimeiva, licha ya ukweli kuwa huenda wamewahi kuwasiliana kabla ya hapo.

Baada tu ya show yao ya Leaders wawili hao hawakuwa wachoyo kwa mashabiki wao kuwaonesha kuwa mazungumzo ya kazi za baadaye yameanza.

Wikzid alipost picha akiwa na hitmaker huyo wa Nana na kuandika, “Big up to @diamondplatnumz for the love!! We link up soon!! #OneAfrica.”

Naye Diamond alipost picha akiwa na hitmaker huyo wa Ojuelegba na kuandika, “When they ask you, what was the name of the food you ate in Tanzania… tell them “Ubwabwa na Kuku” @wizkidayo.”

Wizkid atarejea tena December kwenye Fiesta na huenda kile mashabiki wamekililia kwa muda mrefu kati ya mastaa hawa kitakamilika.

About Author

Advertisement

 
Top