Msanii Linah Sanga ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake wa 'No Stress' amefunguka na kuweka sawa kuwa hana ujauzito kama ambavyo baadhi ya watu wanavyoongea kwenye mitandao ya kijamii.
Msaniii Linah
Linah Sanga ameyasema haya kwenye kipindi cha Television moja hapa nchini na kusema huwa anajipanga ndio maana hajawahi kupata ujauzito pia amedai hana tatizo la uzazi kama baadhi ya watu wanavyohisi.
"Mimi nipo vizuri bhanaa sina tatizo la uzazi ila huwa najipanga ndio maana watu hawajahi kuniona nina ujauzito, lakini kwa sasa najiachia sanaa hivyo muda wowote wanaweza kusikia jambo," alisema Linah.
Katika hatua nyingine Linah amefunguka kuhusu wasanii kuhusika katika masuala ya siasa amesema wengi wao walikuwa wakifanya kampeni na wameimba sana katika kampeni hizo ingawa suala la kupiga kura lilikuwa ni siri yao wenyewe, hivyo kila msanii kwa nafasi yake ndiye anajua alimchagua kiongozi gani katika uchaguzi mkuu wa 2015 ambao ulifanyika Oktoba 25.